Pogba alianzisha EPL kwa rekodi tamu

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba ameweka rekodi katika Ligi Kuu ya England kwa kupachika bao la kwanza la msimu mpya wa ligi hiyo.

Pia, Man United imekuwa timu ya kwanza msimu huu kupata penalti tena ya mapema (dakika tatu) kwenye mchezo dhidi ya Leicester City kwenye dimba la Old Trafford mjini Manchester.

Beki wa Leicester City, Daniel Amartey aliunawa mpira kwenye eneo la hatari na mkwaju wa penalti wa Pogba ulimshinda kipa Kasper Schmeichel na kuipa Man United bao la kuongoza.

Katika mchezo huo wa ufunguzi, Kocha Jose Mourinho amemfanya Pogba kuwa nahodha wa Man United. Licha ya kupata bao la mapema, kwenye mchezo huo Leicester City ilionekana kuwa moto na kutengeneza nafasi za mashambulizi pamoja na kumiliki sehemu kubwa ya mchezo. Hata hivyo, mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, Man United ilikuwa mbele kwa bao 1-0.

Dondoo muhimu ufunguzi EPL

Beki wa Leicester City, Daniel Amartey amekuwa mchezaji wa kwanza kwenye Ligi Kuu ya England msimu huu, kusababisha penalti iliyozaa bao la kwanza, lakini pia amekuwa wa kwanza kupewa kadi ya njano katika mchezo wa kwanza msimu huu. Dakika 51. Man United vs Leicester City

Kiungo mpya wa Manchester City, Fred, amekuwa mchezaji wa pili kupewa kadi ya njano kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya England. Dakika 55. Man United vs Leicester City

Beki wa Man United, Luke Shaw amekuwa mchezaji wa pili kufunga bao kwenye mechi ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya England. Dakika 82. Man United vs Leicester City.

VIKOSI:

MANCHESTER UNITED XI: De Gea; Darmian, Bailly, Lindelof, Shaw; Fred, Pogba (c), Pereira; Mata, Sanchez na Rashford.

Subs: Grant, Smalling, Young, Fellaini, McTominay, Martial, Lukaku

 

LEICESTER XI: Schmeichel; Amartey, Morgan (c), Maguire, Chillwell; Ndidi, Silva; Ricardo, Maddison, Gray na Iheanacho.

Subs: Ward, Evans, Fuchs, Iborra, Albrighton, Ghezzal, Vardy