Mashindano ya utangazaji yashika kasi DSJ

Dar es Salaam. Fainali ya mashindano ya utangazaji kwenye chuo cha uandishi  wa habari cha DSJ kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam imeanza kwa washiriki kuchuana kwenye vipengele tofauti.

Vipengele vinavyoshindaniwa katika mashindano hayo ni mtangazaji bora wa michezo, burudani, vipindi maalumu na usomaji wa habari.

Wanaochuana katika vipengele hivyo kwa upande wa michezo ni Jabir Hamis 'kiungo mnyumbulifu', habari ni Dina Mgana, Florian Rutahiwa, Sheila Abdul, Godbless Gaspar, Itika Francis

Burudani ni Ally Chiwaga, Raymond Casto, Jonhson Kayombo, Matilda Peter, Abdan Twamaenk, kipindi maalum ni Clement Robert, Maria Alphonce.

Majaji wa kuu katika mashindano hayo ni Grace Kingalame mtangazaji wa TBC mwenye uzoefu kwa zaidi ya miaka 13 na Godwin  Mawanja wa Efm na TV 1.