Magufuli, Kikwete awaongoza mamia kuaga Mzee Majuto

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli na Rais mstaafu Jakaya Kikwete amewaongoza mamia ya Watanzania kuaga mwili wa marehemu muigizaji wa vichekesho Amri Athumani 'Mzee Majuto” kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.

Mwili wa Mzee Majuto uliwasili Ukumbini hapo saa nane na shughuli ya kuaga ikaanza ikiwemo salamu za rambirambi na dua ya kuombea iliongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.

Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na vya kijamii na viongozi wa dini wameungana na waigizaji wenzake na marehemu pamoja na wananchi kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu.

Mzee Majuto aliaga dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya taifa Muhimbili jijini dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.