SportPesa kunogesha Simba Day

Kampuni ya ubashiri wa matokeo ya SportPesa imepanga kuipatia Simba hundi ya Shilingi 50 Milioni kama zawadi kwa klabu hiyo.
Fedha hizo zitatolewa kabla ya mchezo baina ya Simba na Asante Kotoko katika maadhimisho ya Tamasha la Simba Day.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kampuni hiyo, hundi ya fedha hizo itakabidhiwa na uongozi wa SportPesa kwa ule wa Simba chini ya Kaimu Rais wa klabu hiyo Salim Abdallah 'Try Again'
SportPesa wamekuwa wakiidhamini Simba tangu mwaka 2017 waliposaini mkataba wa miaka mitatu