Wazee wa Simba Ubungo Terminal wanamkwara asikuambie mtu!

Mwenyekiti wa tawi la Ubungo Terminal Ayubu Simba amesema kwa upande wao walijipanga kuhakikisha wanafanya vitu vya tofauti katika wiki yote kama mwendelezo katika miaka yote inayokuja.
Simba alisema kwanza tukio ambalo watahusika nalo ni shughuli za kijamii ambapo Agosti 4 walikwenda kufanya usafi katika Kituo cha Mabasi Yaendayo Mikoani (Ubungo Bus Terminal) ambapo tawi hili lilianzishwa. 
Anasema kwanza kwa upande wao wanashukuru uongozi wa Simba kuweza kuwapatia heshima ya kuwachagua kama tawi bora la mwaka katika tuzo za MO Simba Awards ambazo zilitolewa kwa wachezaji wa wadau wengine wa timun hiyo.
"Heshima kubwa ambayo wametumepatia ya kupata tuzo na limetufanya kuongeza kasi yetu ya kuwepo na Simba kukote ambapo itakwenda kucheza mechi na kutoa mchango wowte ambao upo ndani ya uwezo wetu," alisema.
"Tawi letu tangu kuanzishwa linatimiza miaka kumi na tutafanya sherehe kwa kushirikiana na wachezaji, viongozi na wadau wote wa Simba na baada ya hapo tutakuwa tunafanya matokeo muhimu ya kuisaidia jamii ambayo yatakuwa muendelezo kwetu," alisema Simba.