Simba, Asante Kototo hapatoshi Simba Day

Dar es Salaam. ‘Hayawi hayawi yamekuwa…’ Mashabiki na wanachama Simba wataupamba Uwanja wa Taifa kwa rangi nyekundu na nyeupe wakati timu ya itakapomenyana na Asante Kototo katika tamasha kubwa la Simba Day litakalofanyika uwanjani hapo.
Kutokana na aina ya usajili uliofanywa na Simba baada ya dirisha la usajili la kiangazi kufunguliwe bila shaka mashabiki watakaofika uwanjani watapata burudani ya aina yake.
Licha ya kwamba mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameendelea kuwa na wachezaji wao wote muhimu walioipa ubingwa msimu uliopita, lakini imeongeza wengine zaidi.
Wachezaji hao waliongezwa licha ya baadhi yao kuonekana katika michuano ya Kombe la Kagame lakini ndio watatambulishwa rasmi wakiwa na jezi watakazozitumia katika Ligi na mashindano mengine.
Tamasha la mwaka huu imenonga zaidi baada ya kikosi cha Simba kikiwa chini ya Mbelgiji Partick Aussems na kimesheheni nyota wengi wa kimataifa kitakuwa na kazi moja tu ya kuwafurahisha mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushudia mbinu za Uturuki.
Wachezaji wapya wanasubiri kuonyesha ufundi kwa mara ya kwanza ni kiungo Mzambia Cleus Chama, washambuliaji Meddie Kagere, Adam Salamba, Mohamed Ibrahim, pia beki mkongwe Pascal Wawa jinsi walivyoweza kutengeneza kombinesheni mpya Simba.
Afisa Habari wa Simba, Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kushudia mechi dhidi ya Asante Kotoko mchezo huo utakua maalumu kwaajili ya kutambulisha wachezaji wao pamoja na jezi zao mpya.
"Simba ina kikosi bora naamini mashabiki wataujaza uwanja kwa lengo la kuja kushuhudia kikosi chao kilivyofanya maandalizi mazuri kuelekea msimu mpya wa Ligi na mashindano ya Ligi ya Mabingwa, katika tamasha hilo kutakuwa na utangulizi wa michezo mbalimbali ambapo Dodoma FC watacheza dhidi ya Simba ," alisema Manara.
Viingilio katika tamasha hilo ni Tsh 5,000 kwa mzunguko huku upande wa VIP ‘B’ ikiwa Tsh. 15,000 na Tsh 20,000 kwa VIP ‘A’.
Kikosi kamili cha Asante Kotoko kilichosafariki kutoka Ghana. Makipa: Felix Annan na  Osei Kwame.
Mabeki:  Amos Frimpong, Augustine Sefa, Samuel Frimpong, Wahab Adams, Nafiu Awudu, Emmanuel Owusu na Agyemang Badu.
Viungo: Akwasi Nti, Jordan Opoku, Prince Acquah, Douglas Owusu Ansah, Micheal Yeboah.
Washambuliaji: Osman Ibrahim, Sougne Yacouba, Obed Owusu na Frederick Boateng.