Msosi wa Simba Uturuki usipime

Muktasari:

Kwani maisha wanayoishi huko ndiyo kama unavyoona kwenye picha, wako vizuri. Wanakula msosi wa maana na kufanya mazoezi ya nguvu kuhakikisha watakaporudi nchini kwa ajili ya msimu mpya wasikamatike.

Istanbul: Kikosi cha wachezaji wa Simba ambacho kipo nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine, mambo yao si mchezo.
Kwani maisha wanayoishi huko ndiyo kama unavyoona kwenye picha, wako vizuri. Wanakula msosi wa maana na kufanya mazoezi ya nguvu kuhakikisha watakaporudi nchini kwa ajili ya msimu mpya wasikamatike.
Simba ambao pia ni mabingwa wa ligi kuu msimu uliopita, wameondoka mwishoni mwa wiki iliyopita na wanatarajia kukaa huko kwa kipindi cha wiki mbili.