Msanii Tonto Dikeh abadili jina

Muigizaji mwenye vituko na skendo zisizoisha, Tonto Dikeh ameamua kubadili jina lake na kuanzia sasa ametaka aitwe "King Tonto" tofauti na jina lake lililozoeleka.
Ingawa Dikeh ameshindwa kuweka hadharani sababu za kutaka kuitwa King Tonto, muigizaji huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwajuza mashabiki kuwa waanze kumuita jina lake hilo jipya.
"Rasmi nimebadili jina langu na sasa ninaitwa King Tonto ambalo linanifanya nijisikie vizuri. Tafadhali naomba mkubaliane na mimi kwa hili jina kubwa ambalo ndio nalitunia kwa sasa," aliandika muigizaji huyo.
Uamuzi huo wa Tonto Dikeh ameutoa miezi kadhaa baada ya ndoa yake na Olankule Churchill kuvunjika kutokana na migogoro ya mara kwa mara.