#WC2018: Thibaut Courtois, ndio kipa bora wa Dunia

Muktasari:

Kipa huyo, amekuwa na kiwango bora katika michuano ambapo katika mechi ya kwanza, aliiongoza Ubelgiji kuisulubu Panama 3-0, huku wakiitungua England mara mbili (1-0, 2-0), huku akimzuia mchezaji bora wa mashindano hayo, Harry Kane.

Moscow,Russia. Kipa wa Chelsea na Ubelgiji ameondoka nchini Russia akiwa shujaa na mfalme, licha ya timu yake kushindwa kuingia mechi ya fainali, baada ya kutawazwa kipa bora wa michuano hiyo, iliyomalizika rasmi leo.

Kipa huyo, amekuwa na kiwango bora katika michuano ambapo katika mechi ya kwanza, aliiongoza Ubelgiji kuisulubu Panama 3-0, huku wakiitungua England mara mbili (1-0, 2-0), huku akimzuia mchezaji bora wa mashindano hayo, Harry Kane.

Courtois anayewindwa na Real Madrid, aliwabwaga kipa wa Ufaransa, Hugo Lloris na Kipa wa Croatia, Danijel Subasic. Baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo, Courtois aliandika maneno haya kwenye ukurasa wake wa mtandao wa twitter:

 "Moja ya mafanikio makubwa kabisa katika maisha ya mchezaji ni kutambuliwa na kupewa tuzo, nimefarijika kushinda tuzo ya kipa bora. Ahsanteni sana."

Makipa wengine ambao waliwahi kushinda tuzo hii, ni Kipa wa Ujerumani Manuel Neuer, aliyeishinda mwaka 2014. Wengine ni Iker Casillas, Gianluigi Buffon, Oliver Kahn, Fabien Barthez, na Michel Preud'homme.