#WC2018: Harry Kane abeba tuzo ya mfungaji bora

Muktasari:

Yakiwa ni mashindano yake ya kwanza, Straika wa Tottenham, ameingia katika rekodi kwa kuwa mchezaji wa pili wa England kuwahi kutwaa tuzo hiyo, baada ya Gary Lineker, aliyeitwaa mwaka 1986, alipotupia mabao sita wavuni. Kane alifunga mabao mawili zaidi ya Romelu Lukaku, Kylian Mbappe, Denis Cheryshev, Cristiano Ronaldo na Antoine Griezmann.

Moscow, Russia. Sasa nimeamini ule msemo wa 'its coming home' wajukuu wa Malkia walimaanisha tuzo ya mfungaji bora inaenda London. Ndio, nahodha wa England, Harry Kane ameibuka mfungaji bora wa michuano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia, baada ya kutupia mabao sita wavuni.

Yakiwa ni mashindano yake ya kwanza, Straika wa Tottenham, ameingia katika rekodi kwa kuwa mchezaji wa pili wa England kuwahi kutwaa tuzo hiyo, baada ya Gary Lineker, aliyeitwaa mwaka 1986, alipotupia mabao sita wavuni. Kane alifunga mabao mawili zaidi ya Romelu Lukaku, Kylian Mbappe, Denis Cheryshev, Cristiano Ronaldo na Antoine Griezmann.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, alifunga mabao matatu tu kwa njia ya kawaida huku mengine matatu yakiwa ni penalti. England walimaliz katika nafasi ya nne, baada ya kupigwa 2-0 na Ubelgiji kwa mabao ya Thomas Muernier na Eden Hazard.