Filamu ya ukeketaji Tanzania yaja

Mtayalishaji wa filamu kutoka Ujerumani, Rechor Gil

Muktasari:

Rechor katika muendelezo wa tamasha la kimataifa la Filamu Zanzibar ameona suala la ukeketaji lilinavyowathiri wasichana wengi Tanzania.

Zanzibar. Mtayalishaji wa filamu kutoka Ujerumani, Giselle Portenier ameamua kutengeneza filamu inayohusu masuala ukeketaji kutokana na maisha ya kweli ya jamii za Tanzania.

Rechor katika muendelezo wa tamasha la kimataifa la Filamu Zanzibar ameona suala la ukeketaji lilinavyowathiri wasichana wengi Tanzania.

Dokumentari hiyo aliopa jina la “In the Name of Your Daughter” inatarajiawa kuonyeshwa karibia mikoa yote na kusambazwa duniani ili kupinga masuala ya udhalilishaji wa kinjisia unaoendelea hususan katika jamii za Afrika.

Rose Makole na Neema Chacha ni wasichana waliowakimbia familia zao kutokana na musuala ya ukeketaji wakiwa wadogo kutokana na kupata elimu ya ukeketaji wakiwa shuleni.

Rose, Neema wamesema walikimbia familia zao kwa hofu na kuhifadhiwa nyumba salama ambayo huwapokea watoto waliofanyiwa ukeketaji katika familia zao iliyopo chini ya dawati la Jinsia na watoto Tanzania.

Robi mlezi mkuu wa kituo hicho cha kituo salama kilichopo wilayani Serengeti na Butiama wamenzisha vituo hivyo baada ya kuona watoto wanaotakiwa wanafanyiwa ukeketaji wanahitaji kulindwa, lakini bado imekuwa changamoto.

“Natumai tatizo hili iko siku litakwisha na tayari linaendelea kwisha kidogo kidogo jamii zetu tayari zishaelimika na tunaendelea na elimu hii iko siku wazazi wa hawa watakuja kuwachukua watoto wao” alisema  Robi.

Dokumentari hiyo iliyotengenezwa kwenye mazingira halisi imesharikisha watoto hao ili kusambaza elimu kwa jamii ambayo bado haijaelimika bado kuhusiana na madhara ya ukeketaji kwa jamii za Afrika.