Sunday June 3 2018

 

By Gift Macha

Nakuru: Baada ya kusaini mikataba mipya na Simba, straika wa zamani wa Tanzania

Prisons, Mohammed Rashid na winga, Shiza Kichuya wanatarajiwa kuwasili mjini hapa leo Jumapili ili kuongeza nguvu.

 Rashid aliyefunga mabao 10 msimu uliopita, amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka

mitatu wakati Kichuya amesaini mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia timu

hiyo aliyoshinda nayo taji moja la FA na Ligi Kuu katika miaka yake miwili ya mwanzo.

Meneja wa Simba, Richard Robert alisema Kichuya na Rashid watawasili sambamba na

Mzamiru Yassin kwaajili ya kuwabeba kwenye mechi za michuano ya SportPesa.

 

“Tuna wachezaji 14 hapa hivyo wakiwasili hao watafika 17, wanatosha kwa michuano hii,

tunapaswa kuwaamini tu ili wafanye kazi,” amesema Richard.