Unai Emery ahakikishiwa usajili wa kiwango Arsenal

London, England: Bosi wa Arsenal, Ivan Gazidis amempa mamlaka Kocha Mhispani Unai Emery ya kufanya anachotaka ndani ya klabu hiyo maarufu kama Washika Bunduki wa London.

Lakini, mpango mkubwa wa Emery  ni kukuhakikisha Arsenal inarudisha makali yake kwenye Ubingwa wa EPL na makombe mengine.

Gazidis amemwambia Emery ana mamlaka ya kutumia rasilimali za klabu kwa ajili ya usajili wa kiwango cha juu katika kipindi kipya cha usajili.

Emery mwenye miaka 46 amezungumza kwa mara ya kwanza na wanahabari England jana Jumatano baada ya klabu hiyo kumkabidhi rasmi kijiti kutoka kwa Arsene Wenger.

Kocha huyo amesema, anakabiliwa na changamoto kubwa kwani kumrithi kocha mkubwa kama Wenger inahiji juhudi kubwa.

"Nilikuwa na kazi nzito kabla, lakini nafurahi kazi hii na hasa kuchukua nafasi ya Wenger,"amesema Emery.

Emey alipata nafasi ya kutembelea maeneo yote muhimu kwenye Uwanja wa Emirates pamoja na vyumba vya kubadilishia nguo na mapumziko.