Simba yaikimbia Yanga Morogoro

Muktasari:

  • Simba iliweka kambi ya siku tano mkoani hapa huku wakifanya mazoezi yao kwa kujificha kweny Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Morogoro. Kikosi cha Simba kimeondoka leo Alhamis mchana mjini Morogoro na kurejea Dar es Salaam kwaajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Yanga.

Simba iliweka kambi ya siku tano mkoani hapa huku wakifanya mazoezi yao kwa kujificha kweny Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Wakati wanatoka katika Lodge ya Moro Mount View, waliweka ulinzi mkali huku makomandoo wao wakiwa hawatako kabisa wachezaji wao kuonekana.

Hawakuishia hapo tu kwani baada ya kuona waandishi wanajaribu kupiga picha walisogeza gari karibu na geti ya Lodge hiyo na kubana kabisa wachezaji wao wasipigwe picha.