Kocha Mcongo wa Yanga aanza mambo Moro

Muktasari:

  • Kocha huyo aliingia majira ya saa nane mchana na alikuwa ameongozana na Mwenyekiti wa Mashindano wa Yanga, Hussein Nyika pamoja na mjumbe wake Salum Mkemi.

KOCHA mpya wa Yanga Mcongoman Mwinyi Zahera,  amewasili kwenye kambi yao waliyoweka katika  hoteli ya Kings Way mjini Morogoro.

Kocha huyo aliingia majira ya saa nane mchana na alikuwa ameongozana na Mwenyekiti wa Mashindano wa Yanga, Hussein Nyika pamoja na mjumbe wake Salum Mkemi.

Mkemi na Nyika ambao wanapambana kwa kila namna kuhakikisha Yanga inafanikiwa, walipomfikisha tu waliwasha gari yao aina ya Mercedes Benz na kuondoka zao.

Uongozi wa Yanga umethibitisha kwamba kocha huyo atakuwa na wachezaji wake leo Jumatano jioni katika mazoezi yao yanayoendelea kwenye Uwanja wa Highland hapa Morogoro.

Hata hivyo, Zahera aliyekuwa amevalia vazi la suti  nyeusi, alionekana mwenye kuchoka na safari na alitokea Dar es Salaam.