Hii ya Pogba huwezi kuamini

Muktasari:

Klabu ya Paris Saint-Germain nayo imekuwa katika mkakati mzito wa kumnasa supastaa huyo wa Kifaransa, lakini mwenyewe kaibuka na kueleza kuwa hana mpango wa kuhamia kati ya klabu hizo na mawazo yake yapo kwingine kabisa na taarifa makini zilizopatikana zinasema kuwa Pogba anataka kurudi Juventus.

LONDON, ENGLAND

KATIKA siku za karibuni taarifa kubwa ilikuwa ni bifu kati ya Kocha Jose Mourinho wa Manchester United na nyota wake Paul Pogba na baadaye kukawa na habari mpya kuwa, kiungo huyo anataka kuondoka Old Trafford huku wengi wakitabiri anaweza kuhamia kwa wababe wa La Liga, Barcelona au Real Madrid.

Klabu ya Paris Saint-Germain nayo imekuwa katika mkakati mzito wa kumnasa supastaa huyo wa Kifaransa, lakini mwenyewe kaibuka na kueleza kuwa hana mpango wa kuhamia kati ya klabu hizo na mawazo yake yapo kwingine kabisa na taarifa makini zilizopatikana zinasema kuwa Pogba anataka kurudi Juventus.

Hata hivyo swali pekee ni je klabu hiyo itaweza kutoa kiasi cha Pauni 100 milioni ambazo ndio bei ya Pogba katika soko la sasa?

Ni suala la kusubiri na kuoana.