Chirwa, Tshishimbi wamaliza utata Morogoro

Muktasari:

Wachezaji hao ambao walishindwa kufanya mazoezi ya pamoja na wenzao tangu walipofika Morogoro, walianza rasmi maandalizi ya pamoja na wenzao asubuhi ya leowakijiwinda na mahasimu wao Simba siku ya Aprili 29, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

WACHEZAJI wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa pamoja na Mcongo Papy Tshishimbi wamechelewa kuungana na wenzao katika kambi yao inayoendelea mkoani Morogoro na wakawasili usiku wa kuamkia leo Jumatano.

Wachezaji hao ambao walishindwa kufanya mazoezi ya pamoja na wenzao tangu walipofika Morogoro, walianza rasmi maandalizi ya pamoja na wenzao asubuhi ya leowakijiwinda na mahasimu wao Simba siku ya Aprili 29, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Meneja wa kikosi hicho,  Hafidh Saleh amesema, wachezaji hao walikosekana kwa sababu ya matatizo tofauti ambapo Chirwa yalikuwa ni ya kifamilia na Tshishimbi alikuwa anamalizia matibabu yake.

Yanga inafanya mazoezi  katika Uwanja wa Highland uliopo nje kidogo ya Mji wa Morogoro, lakini wapinzani wao Simba nao wako mkoani Morogoro wakijiandaa na mchezo huo.