Yanga kamili ya Wolaita hii hapa

Muktasari:

  • Yanga na Wolaitta inacheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika na mshindi atakwenda hatua ya makundi. Yanga inahitaji sare au ushindi wa aina yoyote kusonga mbele baada ya mchezo wa kwanza kushinda kwa jumla ya mabao 2-0.

YANGA inaingia uwanjani kukipiga na Wolaitta Dicha muda wowote kuanzia sasa na kwa mara nyingine beki aliyeisumbua ngome ya ushambuliaji wa Wahabeshi hao, Abdallah Shaibu 'Ninja' ameanza.

Kikosi hicho ni pamoja na kipa Mcameroon Youthe Rostand, mabeki wa pembeni kulia ni Hassan Ramadhani 'Kessy' na kushoto Mwinyi Haji, mabeki wa kati ni Abdallah Shaibu 'Ninja',   Kelvin Yondani 'Vidic' wakati viungo ni Mzimbabwe Thabani Kamusoko na Papy Tshishimbi.

Washambuliaji ni pamoja na  Pius Buswita, Obrey Chirwa ambao watacheza kati wakati,  Raphael Daud naYusuph Mhilu watakuwa pembeni kwenye winga.

Wachezaji wa akiba ni pamoja na mlinda mlango, Beno Kakolanya, Juma Abdul, Gadiel Michael, Nadir

Haroub, Said Juma 'Makapu', Juma Mahadhi na Emmanuel Martine.

Yanga na Wolaitta inacheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika na mshindi atakwenda hatua ya makundi. Yanga inahitaji sare au ushindi wa aina yoyote kusonga mbele baada ya mchezo wa kwanza kushinda kwa jumla ya mabao 2-0.