Fainali FA kupigwa Arusha, mshindi wa pili kubeba Sh 10 mil

Muktasari:

  • Hii ni baada ya mchezo wa fainali iliyopita kati ya Simba na Mbao FC  kupigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma  na Wekundu hao wa Msimbazi wakawa mabingwa.

MCHEZO wa fainali wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)  unatarajiwa kuchezwa Juni 2, 2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha,  lakini kumefanyika maboresho kwa mshindi wa pili ambapo safari hii ataondoka na zawadi ya kitita cha pesa kiasi cha Sh. 10 mil.

Hii ni baada ya mchezo wa fainali iliyopita kati ya Simba na Mbao FC  kupigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma  na Wekundu hao wa Msimbazi wakawa mabingwa.

Mbali na mshindi wa pili kuondoka na Sh 10 mil, bingwa atajinyakulia kiasi cha Sh 50 mil, pia zawadi nyingine zitakwenda kwa mchezaji bora, kipa bora na mfungaji bora kila mmoja atapa kiasi Sh 1 mil.

Mashindano hayo pia yatamzawadia mchezaji bora wa mchezo wa fainali kiasi cha shilingi laki tano (500,000).