Majimaji yakalia kooni Mbao

Sunday April 15 2018

 

By Saddam Sadick

Mwanza. Bao la dakika za nyongeza lililofungwa na mshambuliaji wa Majimaji, Marcel Bonaventure limeisaidia timu yake kupata pointi moja baada ya kulazimisha sare 2-2 na Mbao FC leo Jumapili kwenye Uwanja CCM Kirumba, Mwanza.

Wenyeji Mbao walianza mchezo huo kwa kishindo na kupata mabao mawili yaliyofungwa na Boniface Maganga katika dakika ya 60 na 62.

Majimaji ilicharuka na kupata bao la kwanza kupitia kwa  Bonaventure dakika ya 81, kisha kufunga tena la pili na la kusawazisha  dakika za nyongeza, ambalo limeonekana kuwadhohofisha mashabiki wa Mbao.

Kwa matokeo hayo, Mbao wanafikisha pointi 24, huku Majimaji wakifikisha alama 20 baada ya timu zote kucheza mechi 25 hadi sasa.