Mvua yasitisha ligi ya kikapu Dar

Muktasari:

Serikali imetakiwa kumaliza changamoto ya paa la uwanja huo linalopitisha maji kipindi cha mvua.

Dar es Salaam. Mvua iliyonyesha jijini Dar es Salaam leo Jumapili ilitia doa mechi za Ligi ya mpira wa Kikapu mkoa wa Dar es Salaam (RBA) baada ya Uwanja wa Ndani wa Taifa kujaa maji.

 Mabadiliko ya mechi hizo yaliibua sintofahamu kwa baadhi ya timu ambazo ziliiangukia Serikali na kuiomba kumaliza changamoto ya paa la uwanja huo linalopitisha maji kipindi cha mvua.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Moira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BD), Gosbert Boniface alisema mvua ya jana na leo imepangua ratiba ya ligi hiyo.

 "Uwanja umekuwa ukijaa maji mara kwa mara na kuelekea kupangua ratiba yetu, Uwanja wa Ndani una changamotoya kuvuja kila mvua inaponyesha na kusababisha maji kujaa," alisema Boniface.