Pambano la Joshua vs Parker haponi mtu

Bondia Anthony Joshua (28) amejipata kwamba yupo fiti kuhimili raundi 12 jukwaani katika pambano na mpinzani wake Joseph Parker linalotarajiwa kufanyika Jumamosi usiku.

Mpinzani wake, Parker amerusha kombora kwa akidai kwamba hafikirii kuzitumia raundi zote 12 bali anafikiria kumrarua kwa ‘knockout’.

Wababe hao wa ngumi watakutana kwenye Uwanja wa Principality siku ya Jumamosi  ambapo mshindi atakuwa mshindi wa jumla wa mikanda ya uzito wa juu ya IBF,WBA na WBO.

Joshua amekuwa na rekodi nzuri kwenye mapambano yake baada ya kushinda lile la Cardiff dhidi ya Crlos Takan.

Joshua alisema kwamba mpaka sasa anaendelea vyema na mazoezi yake chini ya mkufunzi wake Rob McCracken.