#WC2018: Keka lote kaachiwa mbuzi

Muktasari:

Mbuzi huyo aliyepewa jina la Zabiyaka aliyepo katika mji wa Samara, ambayo ni miongoni mwa miji 11 itakayotumika kwa fainali hizo kule Russia.

Baada ya kushuhudia Samaki aina ya Pweza akitabiri matokeo ya mechi za Kombe la Dunia mwaka 2006 kule Ujerumani, huku Ngamia akitumika kutabiri fainali za mwaka 2010 na kobe akitabiri fainali za mwaka 2014, mwaka huu mpango mzima utatolewa kupitia kwa mbuzi kutabiri mechi hizo.

Mbuzi huyo aliyepewa jina la Zabiyaka aliyepo katika mji wa Samara, ambayo ni miongoni mwa miji 11 itakayotumika kwa fainali hizo kule Russia.

Zabiyaka alipata nafasi hiyo baada ya kuwashinda wanyama wengine kama Mbweha na Tumbiri kwenye kura zilizopigwa za kuchagua mnyama gani atakuwa mtabiri wa mechi za michuano hiyo.

Kinyang’anyiro cha kumpata myama atakayetabiri matokeo ya mechi hizo, kilihusisha viumbe saba kutoka kwenye eneo la kufugia wanyama la mji wa Samara (Samara Zoo).

Viumbe hao ni, Mbuzi (Zabiyaka), Tumbiri (Simon), Ngamia (Lexus), Skunk (Coco), Chatu (Murzik), Mbweha (Richard) na Kuku (Isadora).