Msuva atua Bongo kumsalimia mama

KESHO  asubuhi majira ya saa 02.00 tu, winga Simon Msuva, atakuwa anatua ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam (JNIA)   akitokea Morocco kwa ajili ya mapumziko.

Msuva ambaye anakipiga klabu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco, anakuwa nchini kwa

mapumziko hayo mafupi baada ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya nchini humo kusimama.

Amesema, atakapotua ataeleza maisha yake ya Morocco na anachotarajia kukifanya baada ya hapo, atakwenda kwa mapumziko.

Watanzania na Afrika kwa ujumla, walimfahamu zaidi Msuva kupitia klabu yake ya zamani ya Yanga

aliyoichezea kwa takribani miaka minne pamoja na Taifa Stars.