Nandy awashukuru Watanzania

Dar Es Salaam. Mwanamuziki wa muziki, Nandy amewashukuru wa Tanzania kwa kumpa sapoti na kufanikiwa kushinda tuzo best Female Artist in Eastern Africa Award.

Nandy alishinda tuzo hiyo kwa kuwashinda wanamuziki wenzake Vannesa Mdee na Feza Kessy waliokuwa wakiwania katika kipengele hicho.

"Kiukweli kwanza niwashukuru watanzania kwa kuniwezasha kutwaa tuzo hii, pili niseme tu ukweli nilikuwa nawahofia wanamuziki wenzangu wa Tanzania, Vannesa Mdee na Feza Kessy kwani mmoja angeweza kuibuka.”

Nandy alisema, kama akipata nafasi ya kufanya kazi na mwanamuziki wa nje, yuko tayari kufanya kazi na Wizkid na Yemi Alade kwani wanafanya muziki anaoutaka yeye.

Aidha Nandy alisema, ameshangazwa na watu wa Nigeria kwa kuupa kipaumbele muziki wa Tanzania kwani toka ametua nchini hapo nyimbo nyingi za kibongo zinapigwa kuliko nyimbo zingine.

"Muziki wa Tanzania umefika mbali kabisa, mie nimeshangwa sana nilipotuwa Nigeria, nimekuta nyimbo nyingi za Kibongo za wasanii mbalimbali zinapigwa, kiukweli nimefajirika na naomba tu wasanii wenzangu tunaweza kufika mbali zaidi."

Nandy alisema watu wanashangaa mimi kuongea kiswahili katika  Interviwe iliyofanyika kwenye Red Capert, ile ilikuwa ni kukipa kipaumbele lugha yetu na siyo kwamba sijui Kiingereza mbona wakati wa kupokea tuzo alizungumza Kiingereza.