Mchumba wa Ronaldo atoa picha yake na kichanga mtandaoni

Madrid, Hispania. Siku chache baada ya kujifungua mtoto wa kike, mchumba wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez ametuma picha katika mtandao kijamii akiwa amemshika kichanga chake.

Katika picha hiyo aliweka ujumbe mzito, Rodriguez aliwashukuru madaktari na wauguzi wa hospitali kwa huduma mzuri waliyompa na kujifungua salama.

 "Kuwa mama na kuanza malezi ya mtoto wangu ni jambo linalonifanya nijisikie mtu mwenye furaha isiyokuwa na kifani," aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

"Sasa amepatikana  mtoto Alana Martina wote tunafuraha isiyokuwa na kifani.

"Nataka kutoa shukrani zangu kwa wahudumu wote kwa ungalizi mzuri waliotupatia kabla, wakati na baada ya kujifungua.

"Pia, tunawashukuru marafiki, ndugu na watu wote waliotupigia simu na kututumia ujumbe na wengine kuja kututembelea hapa."