Rhino Rangers yashukuru Yanga ya kimataifa kuwakosa

Dar es Salaam. Timu ya Rhino Rangers imetoka suluhu ya bila kufungana na Yanga kwenye mchezo wao wa kirafiki uliopigwa jana Jumatano.

Timu hiyo ya Tabora ya maafande wa Jeshi la Wananchi Tanzania, ilitoka uwanjani ikiwa haiamini matokeo ya 0-0 kutokana na kucheza timu hiyo kubwa yenye uzoefu wa kimataifa.

Nahodha wa timu ya Rhino Rangers aliwapongeza wachezaji wenzake kutokana na kutoa suluhu na timu kubwa yenye uzoefu.