Msuva ajipigia tu mabao Morocco

Thursday October 12 2017

 

Morroco. Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Difaa El Jadidi, Simon Msuva amefunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu Morocco.

Katika mchezo huo Jadidi ilikubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Chabab Rif El Hoceima katika mashindano ya Kombe la Throne mchezo uliopigwa jana Jumatano.

Bao la Msuva lilishuhudiwa kwenye dakika ya 34 kipindi cha kwanza baada ya kumzidi ujanja kipa wa Chabab.

Ili kusonga mbele kwenye mashindano hayo hatua ya nusu fainali, Jadidi wanahitajika kushinda kwenye mechi ya pili ya marudiano ambayo watakuwa wenyeji wiki ijayo.

Msuva amedhihirisha ubora wake tangu alipoibuka mfungaji bora msimu wa 2016/17 baada ya kuifungia klabu yake ya Yanga mabao 14.