Mwanzo mbaya wa Mwadui, waitisha Azam

Muktasari:

Azam imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara moja na msimu huu imepania kurudia rekodi hiyo

Dar es Salaam. Kocha wa msaidizi wa Azam, Idd Cheche amesema mechi yao dhidi ya Mwadui FC itakuwa ngumu kutokana na mwanzo mbaya wa wapinzani wao.

Cheche alisema anajua Mwadui itapambana hadi tone la mwisho ili kusaka matokeo baada ya kuanza vibaya katika mechi za mwanzo, ilo litawafanya waingie uwanjani kwa jicho la tatu.

"Kikosi chetu kipo vizuri na tayari tunawasisitiza wachezaji kujituma kuonyesha uwezo wao wa kiwango cha juu kama maandalizi ya ndoto ya ubingwa wetu msimu huu."

"Tunahitaji ushindani wa kufanya kikosi chetu kikawa cha kimataifa badala ya kupata mtelemko utakaotutesa kwenye mashindano ya kuwakilisha nchi, tukifanikiwa kutwaa ubingwa," alisema.

Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelu 'Julio' alisema Azam ni timu ya mfano tangu ipande ligi, naamini msimu huu wanaweza wakafanya vema.

"Naamini wakizingatia mikakati yao wanaweza kuwa na jipya licha ya nyota wao kuondoka ndani ya kikosi hicho, waliyopo lazima wajitume kwa bidii,"alisema.