Mabeki hawa watano wa Ligi Kuu Bara kaa nao mbali

Muktasari:

"Katika mabeki niliokutana nao  kutoka timu nyingine hao watano wameleta changamoto kubwa katika ligi kutokana na ubora wao. Ninawaheshimu na ninajifunza vitu vingi kutoka kwao"alisema Morris.

Dar es Salaam. Mchezaji wa Azam, Agrey Morris amesema anavutiwa na mabeki watano kwenye Ligi Kuu Bara ambao ni Juuko Murshid na Method Mwanjali wa Simba, Kelvin Yondani, Nadir Haroub'Canavaro' wa Yanga na Yakub Mohammed wa Azam.
"Katika mabeki niliokutana nao  kutoka timu nyingine hao watano wameleta changamoto kubwa katika ligi kutokana na ubora wao. Ninawaheshimu na ninajifunza vitu vingi kutoka kwao"alisema Morris.
Azam inajiandaa kuikabili Lipuli  Jumapili katika mchezo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Mbagala.