Nahodha wa Mexico atajwa mtandao hatari wa wauza unga duniani

Thursday August 10 2017

 

Mexico. Nahodha wa timu ya Taifa ya Mexico, Rafael Marquez (38) ametajwa na kitengo cha kuzia dawa za kulevya cha Marekani kuwamo kwenye mtandao hatari wa wauza unga duniani.

Marquez amekuwa miongoni mwa watu 21 na pamoja na taasisi 42 zilizotajwa na Kitengo za Upelelezi wa Makosa ya Dawa za Kulevya cha Marekani.

Marquez amewahi kuzichezea klabu za Ulaya zikiwamo Monaco na Barcelona huku akitajwa kuwa kinara kwenye uuzaji wa dawa za kulevya duniani.

Hata hivyo, Marquez ametoa maelezo yake ya awali kwa mwanasheria mkuu nchini Mexico, hata hivyo ofisi hiyo haikuweka wazi kile alichokieleza.