Katibu wa TFF amtembelea nahodha wa Serengeti Boy nyumbani kwake Dodoma

Muktasari:

Ziara hiyo ya Mwesigwa imekuja ikiwa ni wiki moja tangu Waziri Dk.Harrison Mwakiyembe alipomtembelea nahodha huyo.

Dodoma. Katibu Mkuu wa Shirikisho Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa amemtelea nyumbani kwake aliyekua nahodha Serengeti Boys, Issa  Makamba.

Ziara hiyo ya Mwesigwa imekuja ikiwa ni wiki moja tangu Waziri Dk.Harrison Mwakiyembe alipomtembelea nahodha huyo.

Mwesigwa alifika nyumbani kwa nahodha huyo maeneo ya Mlezi/Image na kuzungumza naye ikiwamo kumjulia hali na maendeleo yake ya jeraha lake la mguu.

Akizungumzia ujio wa Mwesigwa, Makamba amesema kama ilivyokua kwa Waziri

Mwakiyembe amefarijika pia na ujio wa kiongozi huyo wa TFF.

"Ni kweli nimefarijika na ujio wa kiongozi wa TFF ameniulizia maendeleo na majeraha tangu niliporudi nchini na hata sasa nikiwa nyumbani Dodoma na ninaendelea vizuri," alisema Makamba.

Makamba aliumia mguu akiwa na kikosi cha Serengeti Boys wakati wa mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya miaka 17, yaliyofanyika nchini Gabon.