Alliance FC yampa Mataka mkataba na lengo la kupanda Ligi Kuu Bara

Muktasari:

Kabla ya Makata kutua klabuni hapo alikuwa akifundisha KMC ya jijini Da er Salaam.

Mwanza. Klabu ya Alliance Fc imemnasa kocha Mbwana Makata kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya msimu ujao wa ligi daraja la kwanza.

Kabla ya Makata kutua klabuni hapo alikuwa akifundisha KMC ya jijini Da er Salaam.

Mwenyekiti wa mashindano ya klabu ya Alliance, Yusuph Budodi alithibitisha kocha huyo kujiunga nao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Alisema Alliance katika msimu uliopita licha ya kufanya vizuri, lakini haikuweza kupanda Ligi Kuu hivyo makubaliano na kocha Makata ni kuhakikisha anaipandisha Ligi Kuu.

Kocha Mataka, alisema yeye uzoefu na uwezo wake ndiyo silaha na kwamba anachohitaji kutoka katika uongozi ni ushirikiano.

Pia, alisema kuwa hata sababu za timu yake aliyotoka ya KMC kushindwa kupanda ligi kuu ni kutokana na siasa na fitina, lakini kuhusu ubora wa kikosi kiufundi kilikuwa kinaridhisha.

"Mimi sina wasiwasi na kazi hii, nina uwezo na uzoefu wa muda mrefu niombe tu ushirikiano kutoka kwa wanachama, mashabiki na viongozi kunipa ushirikiano," alisema Makata.