Hii ya Ndonga ni kali kupigana mapambano manne ndani ya miezi mitatu

Muktasari:

Bondia huyu bwana amejiwekea rekodi ya peke yake kwa kucheza mapambano manne ndani ya siku 90, tena mawili kati ya hayo amepigana ndani ya wiki mbili tu.

Dar es Salaam. Hii inatokea kibongo bongo tu, maana hata kina Floyd Maywether hawawezi kufanya utani kiasi hicho, lakini bondia Mohammed Shaban 'Ndonga' amejaribu.

Bondia huyu bwana amejiwekea rekodi ya peke yake kwa kucheza mapambano manne ndani ya siku 90, tena mawili kati ya hayo amepigana ndani ya wiki mbili tu.

Lakini sasa ili kuthibitisha ngumi sio chai, jamaa kapigika mapambano yote tena kwenye raundi za mwanzo tu ( kwa TKO). Kuna tetesi alikuwa akiangalia 'mshiko' bila kujali afya yake.

"Asipoagalia atakuwa chizi, bondia huwezi kucheza mapambano manne mfululizo, hizo sio ngumi, " alisema rais wa PST aliyeahi pia kuwa bondia wa timu ya taifa, Emmanuel Mlundwa.