Waamuzi wanne katika mpira wa viziwi waacha gumzo michezi ya Umitashumta

Muktasari:

Mechi hiyo ilishudia Njombe ikichapa Manyara kwa mabao 7-0, shukrani kwa mabao ya Gebo Gunena aliyefunga matano dakika ya 12, 23, 56, 67 na 70, Son Kisake dakika ya 78 na Nsajigwa Mwaseba dakika ya 85.

Mwanza. Mashabiki wa soka walifurika kwenye viwanja vya Butimba kushudia mechi ya soka ya viziwi ikichezeshwa na waamuzi wa nne katika mashindano ya Umitashumta.

Mechi hiyo ilishudia Njombe ikichapa Manyara kwa mabao 7-0, shukrani kwa mabao ya Gebo Gunena aliyefunga matano dakika ya 12, 23, 56, 67 na 70, Son Kisake dakika ya 78 na Nsajigwa Mwaseba dakika ya 85.

Mechi hiyo iliaanza na kuchezeshwa na waamuzi  watatu, yaani wa kati na wawili pembeni,

lakini katikati ya mchezo aliongezeka refa mwingine na wadau hao kujawa na mshangao

wakihoji kwanini waamuzi wanakuwa wanne?.

Waamuzi hao kila mmoja alikuwa na vibendera  tofauti kumbe kulikuwa na maana yake ambayo

mashabiki hao hawakujua haraka, jambo lililolazimisha mkufunzi waamuzi kutoa ufafanuzi kuhusu hilo.

Mkufunzi huyo wa Waamuzi Mkoa wa Mwanza, Alfred Rwiza alisema waamuzi wanne kwenye mchezo huo ilitokana na kupungua kwa vibendera vilivyotakiwa.

Alisema kuwa vibendera vilivyokuwa vinatakiwa ni njano kwa upande wa waamuzi wa pembeni na nyekundu na njano kwa refa wa kati.

“Hiyo nyekundu huashiria faulo na njano hutumika kuruhusu mpira kuendelea, kwahiyo yule aliyeongezeka katikati na vibendera vya njano ni kumsaidia huyo mwenzake aliyepungukiwa moja ya rangi,” alisema Rwiza.