Winga wa Lyon ahadithia alivyotua Tusker Kenya

Muktasari:

Kijibwa alikuwa anakosa nafasi ya kucheza katika klabu ya Lyon na ndipo alipoomba barua ya kuachwa timu hiyo na ndipo alipoomba barua ya kuikacha klabu hiyo na kwenda nchi Kenya kwenda kujaribu kucheza soka la kulipwa.

Dar es Salaam. Winga wa zamani wa African Lyon, Abdul Hassan ‘Kijibwa’ amesema kuwa haikuwa rahisi kuingia katika kikosi cha Tusker Fc cha nchini Kenya kutokana na jinsi ambavyo mazingira ya kucheza kikosi hicho yalivyokuwa.

Kijibwa alikuwa anakosa nafasi ya kucheza katika klabu ya Lyon na ndipo alipoomba barua ya kuachwa timu hiyo na ndipo alipoomba barua ya kuikacha klabu hiyo na kwenda nchi Kenya kwenda kujaribu kucheza soka la kulipwa.

Alisema alivyoenda Kenya alikutana na mchujo wa wachezaji wengi kutoka nchi mbalimbali ambao wote walikuwa wanataka kujiunga na klabu hiyo lakini katika majaribio ya siku ya kwanza alifanikiwa kupenya katika mchujo huo.

“Nilipelekwa Kenya na Kocha Aluko alinambia naweza nikapata nafasi sehemu nyingine, nilivyofika nilikutana na mchujo lakini siku ya kwanza tu nilifanikiwa kupita haikuwa rahisi lakini nilifikilia kuwa nikifeli nitakuwa nipo tu kutokana nilikuwa nimeshaomba barua Lyon,”alisema.