Yanga yaivaa Stand United bila Mwandila

Muktasari:

Mwandila ndiye aliyekuwa anakaa benchi kwa kipindi chote ambacho Mwinyo Zahera alikuwa hajapata kibali cha kazi.

Dar es Salaam. Yanga imeshuka uwanjani kukipiga na Stand United bila kocha wake msaidizi, Mzambia Noel Mwandila.

Mwandila alikuwa kocha pekee anayekaimu nafasi ya kocha mkuu tangu aondoke Mzambia mwenzake, George Lwandamina aliyerudi kwenye timu yake ya zamani ya Zesco.

Wakiwa katika maandalizi ya mchezo huo, Kocha Mkuu Mkongo Mwinyi Zahera na meneja wa timu, Nadir Haroub 'Canavaro' ndio walisimamia mazoezi.

Na baada ya hapo, waliokwenda kukaa kwenye benchi la ufundi ni zahera, kocha wa makipa Juma Pondamali, mratibu Hafidh saleh, daktari wa timu Edward Bavu, Cannavaro pamoja na mtunza vifaa Mahmoud Omari.

Hata hivyo, haikufahamika sababu ya kukosekana kwa kocha huyo msaidizi.