Watanzania kuamua Seychelley, Bafana Bafana

Muktasari:

  • CAF imekuwa ikichagua waamuzi bora kutoka katika mataifa mbalimbali kuchezesha michezo hiyo

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Afrika CAF limetaja mwamuzi Mtanzania, Mfaume Ali Nassoro kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 kati ya Seychelles na Afrika Kusini itakayochezwa Uwanja wa Stade Linite Oktoba 16, 2018.

Katika mchezo huo mwamuzi Nassoro atasaidiwa Watanzania wenzake Ferdinand Chacha, msaidizi namba mbili Alli Kinduru na Mwamuzi wa akiba Elly Sasii.

Mtathmini waamuzi anatokea Uganda Ronnie Kalema na Kamishna wa mchezo anatokea France Yves, Jean-Baptiste Etheve.

Pia, CAF limemteua Ahmed Mgoyi kuwa kamishna wa mchezo wa Kufuzu kucheza AFCON 2019 Cameroon, kati ya Malawi na Cameroon mchezo utakaochezwa Oktoba 16, 2018 Kamuzu Stadium Jijini Blantyre.

Naye Leslie Liunda ameteuliwa kuwa mtathmini wa waamuzi mchezo utakaowakutanisha Congo DR na Zimbabwe utakaochezwa Kinshasa Complexe OmniSports Stade Des Martyrs Oktoba 13, 2018.