Watanzania dua zote kwa Z’bar Heroes leo

Muktasari:

  • Z’bar ilitwaa ubingwa wa Kombe la Chalenji 1995 kwa kuifunga Uganda  

 Wakati Zanzibar Heroes ikitarajiwa kushuka uwanjani kuwavaa Uganda katika nusu fainali ya pili ya Kombe la Chalenji leo, Waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo Dk. Harrisson Mwakyembe amewaomba Watanzania kwa ujumla kuiombea dua njema timu hiyo katika mchezo huo.

Dk.Mwakyembe amesema baada ya timu ya Tanzania bara kutolewa katika mashindano hayo Watanzania hususani wa bara na wale waliopo nchini Kenya kuiunga mkono Z’bar Heroes kwani ndio iliyobaki kuiwakilisha nchi.

"Naipongeza  Zanzibar Heroes kwa kufanya vema katika mashindano ya Chalenji yanayoendelea Kenya na pia naomba Watanzania wote kuiombea dua timu hiyo kwenye mchezo wake dhidi ya Uganda leo bila kujali ni bara au visiwani,"alisema Mwakyembe

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo wakati akifungua mashindano ya vyuo vikuu nchini (TUSA) ambayo yameanza rasmi leo katika chuo kikuu Dodoma (UDOM).