Waamuzi wa Mali, Djibouti kuamua Stars, Cape Verde

Muktasari:

  • Tanzania inahitaji kushinda mchezo huo kufufua matumaini yake ya kufuzu wa Afcon 2019

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Afrika CAF limetaja waamuzi kutoka Mali kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 kati ya Cape Verde na Tanzania utakaochezwa kwenye Uwanja wa Estadio National Oktoba 12, 2018.

Katika mchezo huo mwamuzi wa kati atakua Boubou Traore akisaidiwa na Mwamuzi Drissa Kamory Niabe, pamoja Baba Yomboliba na Mwamuzi wa akiba Gaoussou Kane na Kamishna wa Mchezo anatokea G. Equatorial Tadeo Nsue Onva.

Katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Oktoba 16, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa utachezeshwa na waamuzi kutoka Djibouti.

Mwamuzi wa kati atakuwa Souleiman Ahmed Djama akisaidiwa na Farhan Bogoreh Salime, pamoja na Rachid Waiss Bouraleh na Mwamuzi wa akiba Bilal Abdallah Ismael.

Kamishna wa mchezo anatokea Malawi, Maxwell Mtonga, Mtathmini waamuzi anatokea Rwanda, Michael Gasingwa.