#WC2018: Neymar, Coutinho waibeba Brazil

Muktasari:

  • Mashabiki wa Brazil hawatamsahau Phillipe Coutinho ambaye aliweka wavuni bao la kwanza la kuongoza katika dakika za majeruhi, huku mchezo huo ukitawala kuamuliwa teknolojia ya video ambayo imewakosesha nafasi ya mabao vigogo hao wa soka.

Timu ya Brazil imeiadhibu Costa Rica kwa kuigunga  mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi E wa Kombe la Dunia na kufikisha pointi 4 na kuongoza kundi hilo.
Mashabiki wa Brazil hawatamsahau Phillipe Coutinho ambaye aliweka wavuni bao la kwanza la kuongoza katika dakika za majeruhi, huku mchezo huo ukitawala kuamuliwa teknolojia ya video ambayo imewakosesha nafasi ya mabao vigogo hao wa soka.
Brazil walionekana kuwa na kiu ya kuzifumania nyavu mara kadhaa, huku Costa Roca wakijibu mashambulizi mara kwa mara jambo ambalo lilikuwa likiashiria mchezo huo ungemalizika kwa sare. Hii ni kutoka na timu hizo kutofungana hadi inapotimia dakika ya 90 kabla ya mwamuzi kuongeza muda wa ziada.
Brazil walinyimwa penalti dakika ya 77 ambayo ilizimwa na teknolojia ya video, hata hivyo awali mwamuzi aliashiria Neymar alikuwa amechezewa faulo kwenye eneo la hatari.
Dakika sita za nyongeza za mwamuzi ziligeuka neema kwa kikosi hicho cha Brazil ambacho kwa ushindi huo kimefaikisha alama 4 na kufufua matumaini ya kuosnga mbele hatua ya 16 bora kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia.
Wakati mchezo ukiendelea, mashabiki uwanjani hapo walionekana kupaza sauti na wengine kushika vichwa wakihofu kuumia kwa nyota wao Neymar kila alipoanguka chini.
Neymar ameonekana kukibeba kikosi cha timu hiyo baada ya kutengeneza nafasi nyingi za mabao ambapo hata hivyo alikutana na safu ya ulinzi imara ya Costa Rica.
Hadi mwisho wa mchezo, Brazil ilidhihirisha ubora wake baada ya kuwashangaza mashabiki wao baada ya kufunga mabao ya haraka.