#WC2018: Mzigo wa Croatia wauzika sokoni

Muktasari:

  • Mashabiki nchini Russia wamekuwa wakienda na upepo unavyovuma, sasa wanamiminika kwenye maduka mbalimbali kununua jezi kwa ajili ya fainali hiyo ya historia.

Jumapili ndio itakuwa safari ya mwisho iliyoanzishawa pale Moscow Juni 14 baada ya miamba wa soka Croatia na Ufaransa kuthibitisha ubora na kutinga hatua ya fainali kwenye Kombe la Dunia.
Mashabiki nchini Russia wamekuwa wakienda na upepo unavyovuma, sasa wanamiminika kwenye maduka mbalimbali kununua jezi kwa ajili ya fainali hiyo ya historia.
Joto la fainali limeanza kushika kasi, huku mashabiki wakifanya maandalizi yao ya mwisho kabla ya wababe hao wa soka kukamilisha ngwe ya mwisho baada ya kuhimili mikiki tangu hatua ya makaundi, hatua ya 16 bora, robo fainali na nusu fainali.
Takribani mashabiki 10,000 wa Croatia wamezulu Moscow kwa ajili ya kuwaipa nguvu timu yao kwenye mchezo huo wa fainali.
Shabiki mmoja aliyetua nchini humo kutoka Croatia, alisema amekuwa shabiki wa timu hiyo kwa miaka mingi na hivi sasa ametimiza mika 71.
Hivyo ni matumani yake Croatia itaibamiza Ufaransa licha ya kuwa na kikosi ambacho kimesheheni mastaa.
Croatia ilitinga hatua hiyo ya fainali baada ya kuitandika England mabao 2-1 baada ya kuongezewa dakika 30 ambapo awali zilitoshana nguvu dakika 90 zikiwa zimefungana mabao 1-1.