VIDEO: Mambo ya Ali Kiba yaiva ukumbi usipime!

Muktasari:

  • Ali Kiba anamwoa mrembo Amina ambaye anatoka Mtaa wa Kongowea, familia yake ina uhusiano wa karibu na Gavana wa Mombasa, Hassan Joho.

UKUMBI wa Diamond Jubilee wa mjini Mombasa ambako ndipo itafanyika shughuli ya harusi ya msanii wa Bongo Freva Ali Kiba,  unaendelea kupambwa tayari kwa sherehe hizo zitakazofanyika kesho Alhamisi.

Ali Kiba anatarajia kufunga ndoa na mchumba wake, Amina Khaleef  ni mwenyeji wa Mombasa na amsha amsha za ndoa hiyo hapo Mombasa ndiyo zimezidi kupamba moto.

Inadaiwa kuwa tayari Kiba na familia yake ikiwemo mshkaji wake wa karibu, Ommy Dimpoz

pamoja na timu nzima ya Rockstar walitua jana usiku kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Mrembo Amina ambaye anatokea Mtaa wa Kongowea, familia yake ina uhusiano wa karibu na Gavana wa Mombasa, Hassan Joho.

Gavana huyo ambaye awali alikuwa Mbunge wa Kisauni, ambako Amina alikuwa akiishi pia, ni rafiki wa karibu na Kiba.