TFF yatoa ujumbe mzito mazishi ya Bendera

Muktasari:

  • Alisema hayo jana wakati wa mazishi ya Joel Bendera yaliyofanyika Old Korogwe mjini hapa.

Rais wa TFF, Wales Karia amesema kifo cha Joel Bendera kimeleta pengo kubwa katika medani ya soka kwa sababu rekodi yake kwenye timu ya Taifa bado haijavunjwa.

Amesema TFF itahakikisha inamuenzi kwa kufanyika kazi maelekezo yake.

Alisema hayo jana wakati wa mazishi ya Joel Bendera yaliyofanyika Old Korogwe mjini hapa.

Alisema   Bendera pamoja na kushika nyadhifa nyingine za kiserikali lakini hakuacha kushauri masuala ya soka.

"Tutamkumbuka Bendera kwani amekufa akiacha rekodi yake ikiww haijavunjwa" alisema Karia.

Waombolezaji waliuaga mwili wa Bendera uliagwa katika nyumba yake mpya aliyoijenga mtaa wa majengo ambako alipanga kuhamia siku ya Krismasi na amezikwa makaburi ya Kanisa Kuu la Anglikana Old Korogwe.

Viongozi mbalimbali wa kidini, kiserikali na taasisi mbalimbali walijitokeza kumsindikiza Bendera akiwamo Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete.