Straika Mbao aweka rekodi mbili mechi ya Simba

Muktasari:

Simba iliifunga Ruvu Shooting mabao 7-0 ikatika suluhu na Azam kabla ya kuibandua Mwadui mabao 3-0 lakini leo ameweka rekodi kwa kutikisa nyavu za Simba. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 2-2.

Mshambuliaji wa Mbao FC, Habib Kiyombo ameweka rekodi mbili, kuwa mchezaji wa kwanza kutikisa nyavu za Simba kwani kwa muda mrefu zilikuwa hazijaguswa.

Simba iliifunga Ruvu Shooting mabao 7-0 ikatika suluhu na Azam kabla ya kuibandua Mwadui mabao 3-0 lakini leo ameweka rekodi kwa kutikisa nyavu za Simba. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 2-2.

Rekodi nyingine aliyoweka ni kufunga bao la mapema zaidi, lililofungwa kipindi cha pili dakika moja baada ya kuanza kipindi cha kwanza jana Alhamisi.

Simba imefikisha pointi nane nyuma ya Mtibwa Sugar inayoongoza kwa kuwa na pointi tisa.

Mabao ya Simba yalifungwa na Shiza Kichuya na James Kotei na bao jingine la Mbao lilifungwa na Emmanuel Mvuyekule.