Ronaldinho kuoa wachumba wake wawili

Muktasari:

Watu hao watatu, ambao wamekuwa wakiishi kwa amani kwenye jumba la kifahari la nyota huyo wa soka jijini Rio de Janeiro tangu Desemba mwaka jana, wamepanga kufunga ndoa katikati ya mwaka huu kwa kufanya sherehe moja, kwa mujibu wa gazeti la O Dia la Brazil.

Ndoa za wanawake wengi, zinazidi kuongezeka na kundi kundi moja limepanga kurasimisha mahusiano yao ya kimapenzi; gwiji wa soka wa Brazil na 'wachumba' zake wawili, Priscilla Coelho na Beatriz Souza.

Watu hao watatu, ambao wamekuwa wakiishi kwa amani kwenye jumba la kifahari la nyota huyo wa soka jijini Rio de Janeiro tangu Desemba mwaka jana, wamepanga kufunga ndoa katikati ya mwaka huu kwa kufanya sherehe moja, kwa mujibu wa gazeti la O Dia la Brazil.

 Imeripotiwa kuwa Ronaldinho alianza mapenzi na Coelho miaka michache iliyopita kabla ya kumuona Souza mwaka 2016.

Wanawake hao wameripotiwa kuwa wanapokea "posho" ya dola 2,000 za Kimarekani kutoka kwa Ronaldinho na amekuwa akiwapa zawadi zinazolingana, yakiwamo manukato yanayofanana. Ronaldinho hajawahi kuthibitisha uhusiano wake na wapenzi hao wawili, lakini husafiri nao karibu katika matukio yote anayoalikwa, limesema gazeti la O Dia.

Ndoa za wanawake wengi hazikubaliki kisheria nchini Brazil. Hata hivyo, kuna waliowahi kufanya hivyo: Watu watatu waliingia kwenye uhusiano wakijamii mwaka 2012 nchini Brazil na kuruhusiwa. (Sababu za kuwaruhusu ni kwamba watu hao watatu hawakuwa na haki ya ndoa, bali waliruhusiwa kutumia anuani moja na akaunti moja ya benki).

Ronaldinho na wachumba hao wawili wamepanga kufunga ndoa yao mwezi Agosti.

Chanzo: Yahoo Lifestyle