Prisons yajipanga kuipapasa Ruvu Shooting

Muktasari:

  • Timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza ilianza Ligi Kuu msimu huu vibaya baada ya kupokea vipigo mfululizo katika michezo miwili ya ugenini dhidi ya Simba na Mtibwa Sugar.
  • Hata hivyo ikazindukia nyumbani katika mchezo wa tatu baada ya kuichapa Alliance FC mabao 2-0 hivyo kurejesha morali ya kikosi hicho.

Dar es Salaam. Beki wa Prisons, Laurian Mpalile amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata ushindi wa pili nyumbani dhidi ya Ruvu Shooting.

Prisons itaikaribisha Ruvu Shooting Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza ilianza Ligi Kuu msimu huu vibaya baada ya kupokea vipigo mfululizo katika michezo miwili ya ugenini dhidi ya Simba na Mtibwa Sugar.

Hata hivyo ikazindukia nyumbani katika mchezo wa tatu baada ya kuichapa Alliance FC mabao 2-0 hivyo kurejesha morali ya kikosi hicho.

"Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu  ya kuikabili Ruvu Shooting Jumamosi.

"Ushindi wa mechi iliyopita umetupa morali ya kuendelea kufanya vizuri na hasa kuhakikisha hatupotezi michezo yetu tutakayocheza nyumbani" alisema Mpalile.

"Tunajua mechi itakuwa ngumu kwani Ruvu Shooting ni timu nzuri pia tutapambana tupata ushindi.”