'Okwi' wa Copa Umisseta ni moto

Monday June 11 2018

 

By Imani Makongoro

Mwanza. Kule kwenye mashindano ya Copa Coca Cola Umisseta kuna mchezaji kufunga hat-trick kwake siyo ishu hali iliyopelekea apachikwe jina la nyota wa kimataifa wa Simba, Emmanuel Okwi.


Chipukizi Joyce Meshack anayeuwakilisha mkoa wa Dar es Salaam katika mashindano Umisseta amekuwa gumzo kutokana na uwezo weka mkubwa wa kuzifumania nyavu umeibeba Dar es Salaam kutinga robo fainali.


Joyce anakwambia kiatu cha dhahabu msimu huu hakiendi popote zaidi ya Dar es Salaam licha ya kwamba katika hat-trick zote alizopiga hajawahi kupewa mpira wake na hadi sasa ana mabao 10 katika mechi nne alizocheza