Nani kasema Nsajigwa hajui ‘umombo’? Utapotea

Muktasari:

  • Cheki hii, wakati wanazungumzia mchezo huo, si akatokea jamaa mmoja Mwandishi wa Habari wa Ethiopia akamtwanga swali kwa Lugha ya Kiingereza sasa wakati anataka kujibu akauliza wajumbe ajibu kwa lugha gani.

WATU wana makusudi acha, unajua kilichomtokea Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa baada ya mchezo wao na Welaitta Dicha ya Ethiopia?

Cheki hii, wakati wanazungumzia mchezo huo, si akatokea jamaa mmoja Mwandishi wa Habari wa Ethiopia akamtwanga swali kwa Lugha ya Kiingereza sasa wakati anataka kujibu akauliza wajumbe ajibu kwa lugha gani.

Si unajua Wabongo bwana, wakati anauliza hivyo basi waliangua cheko la maana. Walicheka sana na kumwambia ajibu kwa Kiingereza ili tu wajue anajua au ndiyo walewale ‘tiatia maji’ yaani hawajui Kiingereza.

Kwa makusudi na yeye anajibu vizuri kwa Kiingereza na alipomaliza sasa wakati anatoka nje, Nsajigwa alicheka sana na kutamba akisema: “Hawa jamaa bwana hawa, yaani walijua mimi sijui Kiingereza nini, niko vizuri.”

Kauli ya Nsajigwa kutamba ilikuwa ni faraja kwake kwani sehemu kubwa ya makocha wanapopewa maswali ya Kiingereza huwa wanatetemeka kujibu na mwisho wa siku wanajikuta wanakosea.