Martial hasira kibao kisa Arsenal

Muktasari:

Mfaransa huyo amechoshwa na kitendo cha kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho msimu huu na jambo hilo limemfanya Martial kugoma kusaini dili jipya la miaka mitano la kuendelea kuichezea Man United.

LONDON,ENGLAND

FOWADI wa Manchester United, Anthony Martial ameripotiwa kuchukia baada ya kunyimwa nafasi ya kwenda kuzungumza na Arsenal kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo katika dirisha la Januari.

Mfaransa huyo amechoshwa na kitendo cha kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho msimu huu na jambo hilo limemfanya Martial kugoma kusaini dili jipya la miaka mitano la kuendelea kuichezea Man United.

Katika usajili wa Januari, Man United ilikuwa tayari kuipa Arsenal, Martial, kabla ya baadaye kuamua kumtumia Henrikh Mkhitaryan katika dili la kumsajili Alexis Sanchez. Martial amechukizwa kugomewa kujiunga na Arsenal hasa baada ya usajili wa Sanchez kumfanya akose nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Kocha Mourinho sasa anaweza kukaribisha ofa za kumuuza Mfaransa huyo katika dirisha lijalo la usajili huku klabu kibao ikiwamo Juventus, Arsenal na Olympique Lyon zikionekana kuhitaji huduma ya staa huyo wa zamani wa AS Monaco.